Facebook

SERIKALI IMEMUHAMISHA SAMUEL SITTA,KWENYE NYUMBA ALIOKUWA ANAISHI.


spika wa bunge mstaafu, Samuel Sitta

ALIYEKUWA Spika wa Bunge la tisa, Samuel Sitta, ameondolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi baada ya Serikali kugoma kumlipia kodi ya pango.

Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, mwanasiasa huyo mashuhuri, aliondolewa katika nyumba hiyo iliyopo Masaki, Dar es Salaam na kulazimika kuanza kuhamisha vyombo vyake tangu Ijumaa ya Julai 8, mwaka huu.

Kwa muda wote tangu akiwa Spika wa Bunge, Serikali ilikuwa inalipa kiasi cha dola 8,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh milioni 12 kwa ajili ya nyumba hiyo.

Sitta ambaye baadaye alikuwa waziri katika Wizara ya Afrika Mashariki pamoja na Uchukuzi, aliendelea kuishi katika nyumba hiyo kwa nafasi yake.

Kwa mujibu wa kijana aliyekuwa nyumbani hapo, alisema walianza kuhama tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na wanaendelea kuhama kwa kuhamisha vitu kidogo kidogo.









Alipotafutwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kupitia simu yake yakiganjani, ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema: “Ufafanuzi kuhusumalipo kwa viongozi wastaafu unatolewa kwa viongozi husika na si kwa vyombo vyahabari.”Hali hiyo ya Sitta, imekuwa ni tofauti na aliyekuwa Spika wa Bunge la 10, AnneMakinda, ambaye Serikali kupitia Bunge iligharimia matengenezo ya nyumba yakeiliyoko Kijitonyama, Dar es Salaam, ambako ujenzi wake ulikumbana na lawama kaliza wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo.Spika Makinda alilaumiwa na majirani zake kwa kusababisha usumbufu baada yakuziba njia inayopita katika eneo hilo kwenda maeneo ya Sinza.Kwa mujibu wa Margaret Sitta ambaye ni mke wa Samweli Sitta na  Mbunge waUrambo, alisema kuwa walikuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo ya Serikali kwa kuwamumewe alikuwa Waziri wa Uchukuzi, lakini Baraza la Mawazili lilivunjwa tangumwaka jana hivyo walipaswa kuhama
.Chanzo: Mtanzania
SERIKALI IMEMUHAMISHA SAMUEL SITTA,KWENYE NYUMBA ALIOKUWA ANAISHI. SERIKALI IMEMUHAMISHA SAMUEL SITTA,KWENYE NYUMBA ALIOKUWA ANAISHI. Reviewed by Alex Sonna on 09:20 Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.