Polisi wa mjini Wuerzburg wameeleza kwenye ukurasa wao wa
Facebook kuwa abiria watatu wamejeruhiwa vibaya na wengine 14 wanapata
msaada wa kitabibu kutokana mshtuko walioupata.
Polisi wamesema bado hakuna taarifa yeyote kuhusu sababu ya kutekelezwa kwa shambulio hilo.
vyombo
vya habari vya Ujerumani vimemnukuu msemaji wa wizara ya mambo ya ndani
mjini Bavaria kuwa mtu huyo ni mvulana wa miaka 17, mkimbizi mwenye
asili ya Afghanistan.
Mwaka jana Ujerumani iliwaandikisha
wahamiaji milioni moja waliokuwa wakiingia nchini humo, zaidi ya 150,000
raia wa Afghanistan.
Tangu mashambulizi ya hivi karibuni ya
wanamgambo wa kiislamu nchini Ufaransa, kumekuwa na hali ya hofu ya
kutokea mashambulizi kama hayo nchini Ujerumani, lakini mpaka sasa
hakuna ishara zozote kuwa shambulio hilo lilikua la kigaidi.
ABIRIA WASHAMBULIWA NDANI YA TRENI.
Reviewed by Alex Sonna
on
09:17
Rating:
Reviewed by Alex Sonna
on
09:17
Rating:


Hakuna maoni: