Chama Cha Alliance For Democratic
Change (ADC) kimeadhimisha miaka mitano tangu
kuanzishwa kakwe kwa
kutembelea ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
Katibu Mkuu wa Chama hicho
Doyo Hassan Doyo ameyasema hayo mapema leo hii wakati akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam na kueleza kuwa wamefarijika
kwa kupokewa vizuri katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa japokuwa hawakumkuta.
Pia amefafanua kuwa katika
maadhimisho hayo watatembelea taasisi mbalimbali, magereza,mahabusu ya
watoto, Hospitali ya Taifa Muhimbili kwenda kutoa damu na viomgozi wa
dini.
“katika msafara huu
nimeambatana na wajumbe zaidi ya 14 wakiwemo Mkurugenzi wa Ulinzi na
Usalama,Kamishna Mkuu wa Makao Makuu, Mwenyekiti wa Katiba na Sheria wa
chama, Mwenyekiti wa Taifa wa Vijana,Mkurugenzi wa Habari, Wazee wa
chama na maafisa mbalimbali”,amesema Doyo.
Hata hivyo chama cha ADC wameomba
kwa kipindi hiki cha miaka mitatu iliyobaki Mhe Rais aweze kuwaruhusu
kufanya mikutano ya kisiasa iliwaweze kukuza demokrasia na kuongeza
wanachama kwani chama hicho hakina mbunge wala diwani.
Aidha chama cha ADC
kinatarajia kuanza ziara kwa kutembelea vyombo mbalimbali vya habari
hapo kesho mpaka tarehe 30 ya mwezi huu.
Raufa Mrope,Dar es salaam.
ZIARA YA CHAMA CHA ADC KWA MHE.MAKONDA HII LEO
Reviewed by Alex Sonna
on
06:42
Rating:

Hakuna maoni: