Mshikeshike
wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2016-2017
utakaoshirikisha jumla ya timu 16 kuanza rasmi mwezi wa nane tarehe 20.
Ligi
hiyo inayosimamiwa na shirikisho la soka Tanzania [TFF] kwa udhamini wa
kampuni ya simu ya Vodacom na Azam Media kabla ya ufunguzi Augusti
20,itatanguliwa na mechi ya ngao ya jamii kati ya Yanga na Azam FC
mchezo huu unatarajiwa kuchezwa August 17.
Katika
mechi za ufunguzi Augusti 20,timu zitafungua dimba katika viwanja
mbalimbali nyasi kuwaka moto mjini Bukoba wenyeji Kagera watakuwa
Kaitaba kucheza na Mbeya City,Simb watakuwa Taifa kucheza na Ndanda na
Katika uwanja wa CCM Kirumba Toto Africa watacheza Mwadui.
Katika
uwanja wa Kambarage Mjini Shinyanga wapiga dembe Stand United watacheza
na Mbao FC,Mtibwa Sugar watacheza na Ruvu Shooting katika uwanja wa
Manungu,Songea watakuwa nyumbani katika uwanja wa Samora mjini Songea
watawaalika Tanzania Prinsons na mchezo kati ya Azam dhidi ya African
Lyon utachezwa tarehe 21 katika uwanja wa Azam Complex.
Mechi
ya Yanga dhidi ya JKT Ruvu imepangwa kuchezwa tarehe 31 lakini
wanajangwani hao watacheza tarehe 28 August na African Lyon.Kwani mechi
ya mzunguko wa kwanza inapisha ratiba ya kombe la shirikisho hivyo
mabingwa hao watetezi wataicheza kama kiporo kwa mujibu wa ratiba hiyo.
Timu tatu ambazo zimepanda kutoka ligi daraja la kwanza na kuingia ligi kuu ni Ruvu Shooting,African Lyon na Mbao FC.
Hii Hapa Ratiba Ya Vodacom Ligi Kuu Tanzania Bara 2016-2017.
Reviewed by Alex Sonna
on
22:58
Rating:
Reviewed by Alex Sonna
on
22:58
Rating:


Hakuna maoni: